Zaburi 6:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unigeukie, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe; unisalimishe kwa sababu ya fadhili zako. Biblia Habari Njema - BHND Unigeukie, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe; unisalimishe kwa sababu ya fadhili zako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unigeukie, ee Mwenyezi-Mungu, uniokoe; unisalimishe kwa sababu ya fadhili zako. Neno: Bibilia Takatifu Geuka, Ee Mwenyezi Mungu, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. Neno: Maandiko Matakatifu Geuka Ee bwana, unikomboe, uniokoe kwa sababu ya fadhili zako. BIBLIA KISWAHILI BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu, Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako. |
Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka.
Nitakuwa na wasiwasi rohoni mwangu hadi lini, Nikihuzunika moyoni mchana kutwa? Adui yangu atatukuka juu yangu hadi lini?
Inuka, Ee BWANA, umkabili, umwangushe, Kwa upanga wako uniokoe nafsi yangu na mtu mbaya.
Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.
Tazama; nilikuwa na uchungu mwingi kwa ajili ya amani yangu; Lakini kwa kunipenda umeniokoa kutoka kwa shimo la uharibifu; Kwa maana umezitupa dhambi zangu zote nyuma yako.
Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.
Tokea siku za baba zenu mmegeuka upande, mkayaacha maagizo yangu, wala hamkuyashika. Nirudieni mimi, nami nitawarudia ninyi, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mwasema, Turudi kwa namna gani?