Abrahamu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.
Zaburi 6:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Unihurumie, ee Mwenyezi-Mungu, nimeishiwa nguvu; uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nataabika mpaka mifupani. Biblia Habari Njema - BHND Unihurumie, ee Mwenyezi-Mungu, nimeishiwa nguvu; uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nataabika mpaka mifupani. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Unihurumie, ee Mwenyezi-Mungu, nimeishiwa nguvu; uniponye, ee Mwenyezi-Mungu, nataabika mpaka mifupani. Neno: Bibilia Takatifu Unirehemu Mwenyezi Mungu, kwa maana nimedhoofika; Ee Mwenyezi Mungu, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. Neno: Maandiko Matakatifu Unirehemu bwana, kwa maana nimedhoofika; Ee bwana, uniponye, kwa maana mifupa yangu ina maumivu makali. BIBLIA KISWAHILI BWANA, unifadhili, maana ninanyauka; BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika. |
Abrahamu akamwomba Mungu, Mungu akamponya Abimeleki, na mkewe, na wajakazi wake, nao wakazaa wana.
Nimemwagika kama maji, Mifupa yangu yote imeteguka, Moyo wangu umekuwa kama nta, Na kuyeyuka ndani ya moyo wangu.
Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.
Hamna uzima katika mwili wangu Kwa sababu ya ghadhabu yako. Wala hamna amani mifupani mwangu Kwa sababu ya hatia zangu.
akawaambia, Kwamba utaisikiza kwa bidii sauti ya BWANA, Mungu wako, na kuyafanya yaliyoelekea mbele zake, na kutega masikio usikie maagizo yake, na kuzishika amri zake, mimi sitatia juu yako maradhi yoyote niliyowatia Wamisri; kwa kuwa Mimi ndimi BWANA nikuponyaye.
Uniponye, Ee BWANA, nami nitaponyeka; uniokoe, nami nitaokoka; kwa maana wewe ndiwe uliye sifa zangu.
Njooni, tumrudie BWANA; maana yeye amerarua, na yeye atatuponya; yeye amepiga, na yeye atatufunga majeraha yetu.
Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa wagonjwa, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.
Fahamu sasa ya kuwa Mimi, naam, Mimi ndiye, Wala hapana Mungu mwingine ila Mimi; Naua Mimi, nahuisha Mimi, Nimejeruhi, tena naponya; Wala hapana awezaye kuokoa katika mkono wangu,