na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi;
Zaburi 6:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, usinikemee katika hasira yako, wala usiniadhibu katika ghadhabu yako. BIBLIA KISWAHILI BWANA, usinikemee kwa hasira yako, Wala usinirudi kwa ghadhabu yako. |
na Zekaria, na Yaasieli na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu, na Maaseya, na Benaya, wenye vinanda vya sauti ya Alamothi;
na Metithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, na Azazia, wenye vinubi vya sauti ya Sheminithi,
Tuokoe, ee BWANA, maana hamna tena amchaye Mungu Maana waaminifu wametoweka katika wanadamu.
Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Uliniokoa nilipokuwa katika shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.
Kwa maana jambo hili limekuwa kama maji ya Nuhu kwangu; maana kama nilivyoapa ya kwamba maji ya Nuhu hayatapita juu ya dunia tena, kadhalika nimeapa ya kwamba sitakuonea hasira, wala kukukemea.
Kwa kuwa sitashindana na watu siku zote, wala sitakuwa na hasira siku zote; maana roho ingezimia mbele zangu, na hizo nafsi nilizozifanya.
Usiogope wewe, Ee Yakobo, mtumishi wangu, asema BWANA; kwa maana mimi ni pamoja nawe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokufukuza, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.