Zaburi 59:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu; maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu. Biblia Habari Njema - BHND Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu; maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitakungoja, ewe uliye nguvu yangu; maana wewe, ee Mungu, u ngome yangu. Neno: Bibilia Takatifu Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, Neno: Maandiko Matakatifu Ee nguvu yangu, ninakutazama wewe, wewe, Ee Mungu, ndiwe ngome yangu, BIBLIA KISWAHILI Ee nguvu zangu, nitakungoja Wewe, Maana Mungu ndiye aliye ngome yangu. |
BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu, Nimwogope nani? BWANA ni ngome ya uzima wangu, Nimhofu nani?
Ee nguvu zangu, nitakuimbia sifa, Maana Ewe Mungu ndiwe ngome yangu, Mungu wa fadhili zangu.
Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu; Nitatumaini wala sitaogopa; Maana BWANA YEHOVA ni nguvu zangu na wimbo wangu; Naye amekuwa wokovu wangu.
bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.
ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.
MUNGU, aliye BWANA, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu. [Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele. Amina.]