Zaburi 59:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu. Biblia Habari Njema - BHND Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama! Wananivizia waniue; watu wakatili wanachochea ugomvi dhidi yangu. Neno: Bibilia Takatifu Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee Mwenyezi Mungu, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama wanavyonivizia! Watu wakali wananifanyia hila, ingawa Ee bwana, mimi sijakosea wala kutenda dhambi. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu. |
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego; Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya; Na kufikiri hila mchana kutwa.
Wanaonichukia bure ni wengi Kuliko nywele za kichwa changu. Watakao kunikatilia mbali ni wengi, Adui zangu kwa sababu isiyo kweli. Hata mimi nililipishwa kwa nguvu Vitu nisivyovichukua.
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Basi wewe usikubali; kwa maana watu zaidi ya arubaini wanamwotea, wamejifunga kwa kiapo wasile wala wasinywe hadi watakapomwua; nao sasa wako tayari, wakisubiri kusikia utasemaje.
Kisha Sauli akasema na mwanawe Yonathani, tena na watumishi wake wote, kwamba wamwue Daudi.
Tena, baba yangu, tazama, tafadhali, tazama upindo wa vazi lako mkononi mwangu; maana ikiwa nimeukata upindo wa vazi lako, nisikuue, ujue, na kuona ya kuwa hakuna uovu wala kosa mkononi mwangu, wala sikukukosa neno; ingawa wewe unaniwinda roho yangu ili kuikamata.
Akamwambia Daudi, Wewe u mwenye haki kuliko mimi; maana wewe umenitendea mema, nami nimekutenda mabaya.
Akasema, Bwana wangu ananiwinda mimi mtumishi wake kwa sababu gani? Nimefanya nini mimi? Ni uovu gani nilio nao mkononi mwangu?