Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Zaburi 59:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu; unikinge na hao wanaonishambulia. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu; unikinge na hao wanaonishambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mungu wangu, uniokoe na maadui zangu; unikinge na hao wanaonishambulia. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, uniokoe na adui zangu, unilinde kutokana na hao wanaoinuka dhidi yangu. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu wangu, uniponye na adui zangu, Uniinue juu yao wanaoshindana nami. |
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.
Huniponya na adui zangu; Naam, waniinua juu yao walioniinukia, Na kuniponya na mtu mjeuri.
Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.
Kwa kuwa amekaza kunipenda Nitamwokoa; na kumweka palipo juu, Kwa kuwa amenijua Jina langu.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.