Zaburi 57:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amka, ee nafsi yangu! Amkeni, enyi kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko! Biblia Habari Njema - BHND Amka, ee nafsi yangu! Amkeni, enyi kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amka, ee nafsi yangu! Amkeni, enyi kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko! Neno: Bibilia Takatifu Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. Neno: Maandiko Matakatifu Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. BIBLIA KISWAHILI Amka, ee moyo wangu. Amka, kinanda na kinubi, Nitaamka alfajiri. |
Kwa hiyo moyo wangu unafurahi, Nayo nafsi yangu inashangilia, Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
Amka, amka, jivike nguvu zako, Ee Sayuni; Jivike mavazi yako mazuri, Ee Yerusalemu, mji mtakatifu; Kwa maana tokea sasa hataingia ndani yako Asiyetahiriwa, wala aliye najisi.
Pigeni kelele za furaha, imbeni pamoja, Enyi mahali pa Yerusalemu palipokuwa ukiwa; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Ameukomboa Yerusalemu.
Kwa hiyo moyo wangu ukapendezewa, ulimi wangu ukafurahi; Tena mwili wangu nao utakaa katika matumaini.
Amka, amka, Debora; Amka, amka, imba wimbo. Inuka, Baraka, wachukue mateka wao Waliokuchukua mateka, Ee mwana wa Abinoamu.