Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, angali ni mchanga bado na hana uzoefu, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa BWANA, Mungu.
Zaburi 57:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu! Utukufu wako uenee duniani kote! Biblia Habari Njema - BHND Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu! Utukufu wako uenee duniani kote! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Utukuzwe, ee Mungu, juu ya mbingu! Utukufu wako uenee duniani kote! Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, utukufu wako na uenee duniani kote. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu, Na juu ya nchi yote uwe utukufu wako. |
Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, angali ni mchanga bado na hana uzoefu, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa BWANA, Mungu.
Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu.
Ee, MUNGU, Bwana wetu Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote! Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
Macho ya mwanadamu yaliyoinuka yatashushwa chini, na kiburi cha mwanadamu kitainamishwa, naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Na majivuno ya mwanadamu yatainamishwa, na kiburi cha watu kitashushwa; naye BWANA, yeye peke yake, atatukuzwa siku hiyo.
Basi sasa, BWANA, Mungu wetu, utuokoe kutoka kwa mkono wake, falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA, wewe peke yako.
Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni BWANA wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake.
Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa BWANA;