Zaburi 56:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mungu, uwalipe kwa kadiri ya uovu wao, uwaangushe hao waovu kwa hasira yako. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mungu, uwalipe kwa kadiri ya uovu wao, uwaangushe hao waovu kwa hasira yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mungu, uwalipe kwa kadiri ya uovu wao, uwaangushe hao waovu kwa hasira yako. Neno: Bibilia Takatifu Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. Neno: Maandiko Matakatifu Wasiepuke kwa vyovyote, Ee Mungu, katika hasira yako yaangushe mataifa. BIBLIA KISWAHILI Je! Wataokoka kwa uovu wao? Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako. |
Mauti na iwapate kwa ghafla, Na washuke kuzimu wangali hai, Maana uovu uko nyumbani mwao moyoni mwao.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Hakuna mwenye uwezo juu ya roho aizuie roho; Wala hana mamlaka juu ya siku ya kufa; Wala hakuna kuponyoka katika vita vile; Wala uovu hautamwokoa yule aliyeuzoea.
Kwa sababu mmesema, Tumefanya agano na mauti, tumepatana na kuzimu; pigo lifurikalo litakapopita, halitatufikia sisi; kwa maana tumefanya maneno ya uongo kuwa kimbilio letu, tumejificha chini ya maneno yasiyo kweli;
Hasira yako uwamwagie mataifa wasiokujua, na jamaa zao wasioliitia jina lako; kwa maana wamemla Yakobo, naam, wamemla kabisa na kumwangamiza, na kuyafanya makao yake kuwa ukiwa.
kisha mtakuja na kusimama mbele zangu katika nyumba hii, iitwayo kwa jina langu, na kusema, Tumepona; ili mpate kufanya machukizo hayo yote?
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;