Zaburi 56:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa waliniotea ili waniue. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanakutana kupanga na kunivizia; wanachunguza yote nifanyayo; wananiotea kwa shabaha ya kuniua. Biblia Habari Njema - BHND Wanakutana kupanga na kunivizia; wanachunguza yote nifanyayo; wananiotea kwa shabaha ya kuniua. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanakutana kupanga na kunivizia; wanachunguza yote nifanyayo; wananiotea kwa shabaha ya kuniua. Neno: Bibilia Takatifu Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. Neno: Maandiko Matakatifu Wananifanyia hila, wanajificha, wanatazama hatua zangu, wakiwa na shauku ya kuutoa uhai wangu. BIBLIA KISWAHILI Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu, Kwa kuwa waliniotea ili waniue. |
Wamenifumbulia vinywa vyao; Wamenipiga shavuni kwa kunitukana; Hukutana pamoja juu yangu.
Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Kwa maana wanaiotea nafsi yangu; Wenye nguvu wamepanga kunishambulia; Ee BWANA, si kwa kosa langu, Wala si kwa hatia yangu.
Ewe mtu mbaya, usiyavizie makao yake mwenye haki; Wala usipaharibu mahali pake pa kupumzika;
Tazama, hakika ikiwa utashambuliwa na yeyote, haitakuwa kwa shauri langu. Yeyote atakayekushambulia ataanguka kwa ajili yako.
Maana nimesikia shutuma za watu wengi; hofu ziko pande zote. Rafiki zangu wote, wanaonivizia nisite, husema, Mshitaki, nasi tutamshitaki, huenda akahadaika, nasi tutamshinda, tutajilipiza kisasi kwake.
Basi mawaziri na viongozi wakatafuta sana kupata sababu za kumshitaki Danieli kwa habari za mambo ya ufalme; lakini hawakuweza kuona sababu wala kosa; kwa maana alikuwa mwaminifu, wala halikuonekana kosa wala hatia ndani yake.
Nao waliomkamata Yesu wakampeleka kwa Kayafa, Kuhani Mkuu, walikokuwa wamekutanika waandishi na wazee.
Na ilipokuwa asubuhi, wakuu wa makuhani wote na wazee wa watu wakafanya shauri juu ya Yesu, wapate kumwua;
Wakamviziavizia, wakatuma wapelelezi waliojifanya kuwa watu wa haki, ili wamnase katika maneno yake, wapate kumtia katika enzi na mamlaka ya mtawala.