Zaburi 56:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchana kutwa wanapotosha kisa changu; mawazo yao yote ni ya kunidhuru. Biblia Habari Njema - BHND Mchana kutwa wanapotosha kisa changu; mawazo yao yote ni ya kunidhuru. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchana kutwa wanapotosha kisa changu; mawazo yao yote ni ya kunidhuru. Neno: Bibilia Takatifu Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga njama za kunidhuru. Neno: Maandiko Matakatifu Mchana kutwa wanayageuza maneno yangu, siku zote wanapanga shauri la kunidhuru. BIBLIA KISWAHILI Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu, Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya. |
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Na baadaye wawili wakatokea, wakasema, Huyu alisema, Naweza kulivunja hekalu la Mungu, na kulijenga kwa siku tatu.
akisema juu ya mambo haya kama afanyavyo katika barua zake zote pia, katika barua hizo yamo mambo ambayo ni vigumu kuyaelewa na mambo hayo watu wasio na elimu, wasio imara, huyapotoa, kama vile wapotoavyo Maandiko mengine, na kujiletea maangamizi wao wenyewe.
Kisha Sauli akamwambia Daudi, Tazama, binti yangu mkubwa, Merabu, huyu nitakupa wewe ili umwoe; ila na wewe uniwie hodari wa vita, na kuvipiga vita vya BWANA. Maana Sauli alisema moyoni mwake, Mkono wangu usiwe juu yake, bali mkono wa Wafilisti na uwe juu yake.
Naye Sauli akasema moyoni, Mimi nitamwoza huyu, awe mtego kwake, tena kwamba mkono wa Wafilisti uwe juu yake. Basi Sauli akamwambia Daudi mara ya pili, Leo utakuwa mkwe wangu.
Naye Sauli akazidi kumwogopa Daudi; tangu wakati huo, Sauli akawa adui yake Daudi daima.
Sauli akamtupia mkuki wake ili kumpiga; basi Yonathani akajua ya kuwa baba yake ameazimia kumwua Daudi.
Basi, akisema, Ni vema, mimi mtumishi wako nitakuwa na amani; bali akikasirika, ujue ya kuwa amekusudia kutenda jambo baya.