Zaburi 56:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mungu, unionee huruma, maana watu wananishambulia. Mchana kutwa maadui wananidhulumu. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mungu, unionee huruma, maana watu wananishambulia. Mchana kutwa maadui wananidhulumu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mungu, unionee huruma, maana watu wananishambulia. Mchana kutwa maadui wananidhulumu. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu unihurumie, maana watu wananifuatia vikali; mchana kutwa wanazidisha mashambulizi yao. BIBLIA KISWAHILI Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza, Mchana kutwa ananionea akileta vita. |
Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.
Utawafanya kuwa kama tanuri ya moto, Wakati wa ghadhabu yako. BWANA atawameza kwa ghadhabu yake, Na moto utawateketeza.
Watenda mabaya waliponikaribia, Wanile nyama yangu, Watesi wangu na adui zangu, Walijikwaa wakaanguka.
Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki, Jicho langu limenyauka kwa masumbufu, Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu.
Juu yako adui zako wote Wamepanua vinywa vyao; Huzomea, husaga meno yao, Husema, Tumemmeza; Hakika siku hii ndiyo tuliyoitazamia; Tumeipata, tumeiona.
Bwana ameyameza makao yote ya Yakobo, Wala hakuona huruma; Ameziangusha ngome za binti Yuda Katika ghadhabu yake; Amezibomoa hata nchi Ameunajisi ufalme na wakuu wake.
Bwana amekuwa mfano wa adui, Amemmeza Israeli; Ameyameza majumba yake yote, Ameziharibu ngome zake; Tena amemzidishia binti Yuda Matanga na maombolezo.
Basi huu uharibikao utakapovaa kutoharibika, na huu wa kufa utakapovaa kutokufa, hapo ndipo litakapokuwa lile neno lililoandikwa, Mauti imemezwa katika ushindi.
Lakini wakuu wa Wafilisti wakamkasirikia, na kumwambia, Mrudishe huyu, apate kurejea mahali pake ulipomwagiza, wala asiende pamoja nasi vitani, asije akawa adui wetu vitani; kwani mtu huyu angejipatanisha na bwana wake kwa njia gani? Je! Si kwa vichwa vya watu hawa?