Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa!
Zaburi 55:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wangu umejaa hofu, vitisho vya kifo vimenisonga. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wangu umejaa hofu, vitisho vya kifo vimenisonga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wangu umejaa hofu, vitisho vya kifo vimenisonga. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wangu umejaa uchungu, hofu za mauti zimenishambulia. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wangu umejaa uchungu, hofu ya kifo imenishambulia. BIBLIA KISWAHILI Moyo wangu unaumia ndani yangu, Na hofu za mauti zimeniangukia. |
Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa!
Watesi wangu hunitukana mithili ya kuniponda mifupa yangu, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?
Laumu imenivunja moyo, Nami ninaugua sana. Nikangoja aje wa kunihurumia, wala hakuna; Na wa kunifariji, wala sikumwona mtu.
Sasa roho yangu imefadhaika; nami nisemeje? Baba, uniokoe katika saa hii? Lakini ni kwa ajili ya hayo nilivyoifikia saa hii.
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;