Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
Zaburi 55:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na taabu zimo ndani yake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema vikiuzunguka usiku na mchana, na kuujaza maafa na jinai. Biblia Habari Njema - BHND vikiuzunguka usiku na mchana, na kuujaza maafa na jinai. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza vikiuzunguka usiku na mchana, na kuujaza maafa na jinai. Neno: Bibilia Takatifu Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, uovu na dhuluma vimo ndani yake. Neno: Maandiko Matakatifu Usiku na mchana wanazunguka juu ya kuta zake, uovu na dhuluma vimo ndani yake. BIBLIA KISWAHILI Mchana na usiku huzunguka kutani mwake; Uovu na taabu zimo ndani yake; |
Mtu mmoja akamwambia Daudi ya kwamba, Ahithofeli yu katika hao waliopatana na Absalomu; Daudi akasema, Ee BWANA, nakusihi, uugeuze ushauri wa Ahithofeli uwe ubatili.
BWANA akamwambia, Pita kati ya mji, kati ya Yerusalemu, ukatie alama katika vipaji vya nyuso vya watu wanaopiga kite na kulia kwa sababu ya machukizo yote yanayofanyika kati yake.
Maana wamefanya moyo wao kuwa tayari kama tanuri, wakati waoteapo; hasira yao hulala usiku kucha; asubuhi yawaka kama moto utoao miali.
Mbona wanionesha uovu, na kunifanya nione mabaya? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea.
Kisha wakamchukua Yesu kutoka kwa Kayafa mpaka Praitorio, nayo ikawa alfajiri; lakini wao wenyewe hawakuingia ndani ya ile Praitorio, wasije wakanajisika, bali wapate kuila Pasaka.
Basi Yuda, akiisha kupokea kikosi cha askari na watumishi waliotoka kwa wakuu wa makuhani na Mafarisayo, akaenda huko na taa na mienge na silaha.
lakini hila yao ikajulikana na Sauli. Wakamvizia malangoni mchana na usiku wapate kumwua.
Kisha Sauli akatuma wajumbe mpaka nyumbani kwa Daudi, ili wamvizie na kumwua asubuhi; naye Mikali, mkewe Daudi, akamwambia, akasema, Wewe usipojiponya nafsi yako usiku huu, kesho utauawa.