Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
Zaburi 54:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yeye atawaadhibu maadui zangu kwa uovu wao wenyewe; kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize. Biblia Habari Njema - BHND Yeye atawaadhibu maadui zangu kwa uovu wao wenyewe; kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yeye atawaadhibu maadui zangu kwa uovu wao wenyewe; kwa uaminifu wako, ee Mungu, uwaangamize. Neno: Bibilia Takatifu Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. Neno: Maandiko Matakatifu Mabaya na yawarudie wale wanaonisingizia, kwa uaminifu wako uwaangamize. BIBLIA KISWAHILI Atawarudishia adui zangu ubaya wao; Uwaangamize kwa uaminifu wako. |
Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia, Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.
Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu Unijibu Kwa uaminifu wako, Unijibu kwa haki yako.
Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu; Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi, Kwa maana mimi ni mtumishi wako.
Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
Mpendeni BWANA, Ninyi nyote mlio watauwa wake. BWANA huwahifadhi waaminifu, Bali humlipiza mwenye kiburi ipasavyo.
BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu,
Ee Mungu, wenye kiburi wamenishambulia; Kundi la watu wakatili wanataka kuniua. Wala hawakukuweka Wewe Mbele ya macho yao.
Naye atawarudishia uovu wao, Atawaangamiza katika ubaya wao, Naam, BWANA, Mungu wetu, atawaangamiza.
Iskanda, mfua shaba, alionesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa kulingana na matendo yake.
Mlipeni kama yeye alivyolipa, mkamlipe mara mbili kwa kadiri ya matendo yake. Katika kikombe kile alichokichanganyisha, mchanganyishieni mara mbili.