akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
Zaburi 54:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniokoe, ee Mungu, kwa jina lako; unitetee kwa nguvu yako. Biblia Habari Njema - BHND Uniokoe, ee Mungu, kwa jina lako; unitetee kwa nguvu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniokoe, ee Mungu, kwa jina lako; unitetee kwa nguvu yako. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu uniokoe kwa jina lako, unifanyie hukumu kwa uwezo wako. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu, kwa jina lako uniokoe, Na kwa uweza wako unifanyie hukumu. |
akasema, Ee BWANA, Mungu wa baba zetu, si wewe uliye Mungu mbinguni? Tena si wewe utawalaye falme zote za mataifa? Na mkononi mwako mna uweza na nguvu, asiweze mtu yeyote kusimama kinyume chako.
Ee BWANA, unihukumu mimi, Maana nimekwenda kwa ukamilifu wangu, Nami nimemtumaini BWANA bila wasiwasi.
Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu, Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia. Mkono wako wa kulia umejaa haki;
Ee Mungu wa wokovu wetu, utusaidie, Kwa ajili ya utukufu wa jina lako. Utuokoe, utusamehe dhambi zetu, Kwa ajili ya jina lako.
Mfalme mkuu upendaye hukumu kwa haki; Umeiimarisha haki; Umefanya hukumu na haki katika Israeli.
Jitunzeni mbele yake, muisikize sauti yake; wala msimtie kasirani; maana, hatawasamehe makosa yenu; kwa kuwa jina langu limo ndani yake.
Tazama, jina la BWANA linakuja kutoka mbali sana, linawaka kwa hasira yake, kwa moshi mwingi sana unaopaa juu; midomo yake imejaa ghadhabu, na ulimi wake ni moto uangamizao;
Mkombozi wao ni hodari; BWANA wa majeshi ndilo jina lake; yeye atawatetea kwa bidii, apate kuistarehesha nchi, na kuwasumbua wakaao katika Babeli.
Naye atazaa mwana, nawe utamwita jina lake Yesu, maana, yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.
Tazama, bikira atachukua mimba, Naye atazaa mwana; Nao watamwita jina lake Imanueli; Yaani, Mungu pamoja nasi.
Na ndugu atamsaliti nduguye ili auawe, na baba atamsaliti mwana, na wana watawainukia wazazi wao, na kuwaua.
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Basi hao Wazifi wakamwendea Sauli huko Gibea, wakasema, Je! Yule Daudi hakujificha katika kilima cha Hakila, kuelekea Yeshimoni?