Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Zaburi 52:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Ee Mungu, nitakushukuru daima, kwa ajili ya mambo uliyofanya. Nitatangaza kwamba wewe ni mwema, mbele ya watu wako waaminifu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Ee Mungu, nitakushukuru daima, kwa ajili ya mambo uliyofanya. Nitatangaza kwamba wewe ni mwema, mbele ya watu wako waaminifu.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Ee Mungu, nitakushukuru daima, kwa ajili ya mambo uliyofanya. Nitatangaza kwamba wewe ni mwema, mbele ya watu wako waaminifu.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Nitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda, nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema. Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Nitakushukuru milele kwa maana umetenda; Nitalingojea jina lako kwa kuwa ni jema; Mbele ya wacha Mungu wako.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Zaburi 52:9
17 Marejeleo ya Msalaba  

Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, na pia mambo yote ambayo mfalme amemfanikisha kwayo, na jinsi alivyompandisha cheo juu ya wakuu na watumishi wa mfalme.

Nitamsifu BWANA muda ninaoishi, Nitamwimbia Mungu wangu ningali ni hai.

Umtumainie BWANA, uwe imara, Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.

Ili nafsi yangu ikusifu, Wala isinyamaze. Ee BWANA, Mungu wangu, Nitakushukuru milele.

Nilimngoja BWANA kwa subira, Akaniinamia na kusikia kilio changu.

Kwa ukunjufu wa moyo nitakutolea dhabihu; Ee BWANA, nitalishukuru jina lako, maana ni jema.

Nafsi yangu yamngoja Mungu peke yake kwa utulivu, Wokovu wangu hutoka kwake.

Nafsi yangu, umngoje Mungu peke yake kwa utulivu. Maana tumaini langu hutoka kwake.

Nami kumkaribia Mungu ni kwema kwangu; Nimefanya kimbilio kwa Bwana MUNGU, Niyahubiri matendo yako yote.

Jina la BWANA ni ngome imara; Mwenye haki huikimbilia, akawa salama.