Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 52:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Kwa hivyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyakua na kukuondoa nyumbani mwako; atakungoa katika nchi ya walio hai.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Kwa hivyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyakua na kukuondoa nyumbani mwako; atakungoa katika nchi ya walio hai.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Kwa hivyo Mungu atakuangamiza milele, atakunyakua na kukuondoa nyumbani mwako; atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema lako, atakung’oa kutoka nchi ya walio hai.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hakika Mungu atakushusha chini kwa maangamizi ya milele: atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu kutoka hema yako, atakung’oa kutoka nchi ya walio hai.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Lakini Mungu atakuharibu hata milele; Atakuondolea mbali; Atakunyakua hemani mwako; Atakung'oa katika nchi ya walio hai.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 52:5
18 Marejeleo ya Msalaba  

Atang'olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho.


Nitaenenda mbele za BWANA Katika nchi za walio hai.


Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.


Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.


Mdomo wa kweli utathibitishwa milele; Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.


Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Wala asemaye uongo hataokoka.


Shahidi wa uongo hakosi ataadhibiwa; Naye asemaye uongo ataangamia.


Bali waovu watatengwa na nchi, Nao wafanyao hila watang'olewa.


Nami nitakusukuma na kukutoa katika mahali pako, naye atakushusha utoke hapa usimamapo.


Nilisema, Sitamwona BWANA, yeye BWANA, katika nchi ya walio hai; Sitamwona mwanadamu tena pamoja na hao wakaao duniani.


Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.