Kwa maana vinywa viovu na vyenye hila vimefumbuliwa juu yangu, Vikinisema kwa ulimi wa uongo, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
Zaburi 52:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya. Biblia Habari Njema - BHND Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! Unafikiria tu kutenda mabaya. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila wakati unawaza maangamizi; ulimi wako ni kama wembe mkali! unafikiria tu kutenda mabaya. Neno: Bibilia Takatifu Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mnaofanya hila. Neno: Maandiko Matakatifu Ulimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi. Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila. BIBLIA KISWAHILI Ulimi wako watunga madhara, Kama wembe mkali, Ewe mwenye hila. |
Kwa maana vinywa viovu na vyenye hila vimefumbuliwa juu yangu, Vikinisema kwa ulimi wa uongo, Wamesema nami kwa ulimi wa uongo.
Nafsi yangu i kati ya simba, Nitastarehe kati yao waliowaka moto. Wanadamu meno yao ni mikuki na mishale, Na ndimi zao ni upanga mkali.
Kuna kizazi cha watu ambao meno yao ni panga; Na vigego vyao ni kama visu. Ili kuwala maskini waondolewe katika nchi, Na wahitaji katika wanadamu.
Hapo ndipo waliposema, Njooni na tufanye mashauri juu ya Yeremia; maana sheria haitampotea kuhani, wala shauri halitampotea mwenye hekima, wala neno halitampotea nabii. Njooni, na tumpige kwa ndimi zetu, wala tusiyaangalie maneno yake yoyote.
Basi wakuu wa makuhani na baraza yote wakatafuta ushuhuda wa uongo juu ya Yesu, wapate kumwua;
Baada ya siku tano, Anania, Kuhani Mkuu, akateremka na baadhi ya wazee pamoja naye, na msemi mmoja, Tertulo, nao wakamweleza mtawala habari za Paulo.
Kwa maana tumemwona mtu huyu kuwa mkorofi, mwanzilishi wa fitina katika Wayahudi wote duniani, tena ni kichwa cha madhehebu ya Wanazareti.
Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo.
lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku.
Ndipo akajibu Doegi, Mwedomi, aliyesimama karibu na watumishi wa Sauli, akasema, Mimi nilimwona mwana wa Yese akienda Nobu, kwa Ahimeleki, mwana wa Ahitubu.