Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 51:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Ee Mungu, unirehemu, kulingana na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Nihurumie, Ee Mungu, kadiri ya fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa huruma yako.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Nihurumie, Ee Mungu, kadiri ya fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa huruma yako.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Nihurumie, Ee Mungu, kadiri ya fadhili zako; ufutilie mbali makosa yangu, kadiri ya wingi wa huruma yako.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ee Mungu, unihurumie, kwa kadiri ya upendo wako usiokoma, kwa kadiri ya huruma yako kuu, uyafute makosa yangu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Ee Mungu, unirehemu, Sawasawa na fadhili zako. Kiasi cha wingi wa rehema zako, Uyafute makosa yangu.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 51:1
31 Marejeleo ya Msalaba  

Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari la jumba la mfalme; na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga; naye huyo mwanamke alikuwa mzuri sana, wa kupendeza macho.


wala usiusitiri uovu wao, wala isifutwe dhambi yao, mbele zako; kwa maana wamekukasirisha mbele ya hao wanaojenga.


Akawakumbukia agano lake; Akawahurumia kwa wingi wa fadhili zake;


Baba zetu katika Misri Hawakuzingatia matendo yako ya ajabu; Hawakukumbuka wingi wa fadhili zako; Wakaasi penye bahari, Bahari ya Shamu.


Na Wewe, MUNGU, Bwana, unitendee kwa ajili ya jina lako, Kwa kuwa fadhili zako ni njema uniokoe.


Kama zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako, Na amri zako unifundishe.


BWANA ni mwema kwa watu wote, Na rehema zake ziko juu ya vyote alivyoumba.


Ee Mungu wa haki yangu, uniitikie niitapo; Uliniokoa nilipokuwa katika shida; Unifadhili na kuisikia sala yangu.


Nawe, BWANA, usinizuilie rehema zako, Fadhili zako na kweli yako na zinihifadhi daima.


Bali mimi, kwa wingi wa fadhili zako, Nitaingia nyumbani mwako; Na kusujudu kwa kicho, Nikilielekea hekalu lako takatifu.


Usitiri uso wako usitazame dhambi zangu; Uzifute hatia zangu zote.


Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako.


Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee.


Mungu amesahau fadhili zake? Amezuia kwa hasira rehema zake?


Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe, wala sitazikumbuka dhambi zako.


Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.


Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.


Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.


Lakini wewe, BWANA, unajua mashauri yao yote juu yangu, ya kuniua; usiwasamehe uovu wao, wala usifute dhambi yao mbele za macho yako; bali wakwazwe mbele zako; uwatende mambo wakati wa hasira yako.


Maana ajapomhuzunisha atamrehemu, Kwa kadiri ya wingi wa huruma zake.


Ee Mungu wangu, tega sikio lako, ukasikie; fumbua macho yako ukautazame ukiwa wetu, na mji ule ulioitwa kwa jina lako; maana hatukutolei maombi yetu kwa sababu ya haki yetu, lakini kwa sababu ya rehema zako nyingi.


Rehema na msamaha ni kwa Bwana Mungu wetu, ingawa tumemwasi;


Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;


akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani;