BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Zaburi 50:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana kila mnyama-pori ni wangu, Na mifugo juu ya angani elfu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Biblia Habari Njema - BHND maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza maana wanyama wote porini ni mali yangu, na maelfu ya wanyama milimani ni wangu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana kila mnyama wa msituni ni wangu, na pia makundi ya mifugo juu ya vilima elfu. BIBLIA KISWAHILI Maana kila mnyama-pori ni wangu, Na mifugo juu angani maelfu. |
BWANA Mungu akafanyiza kutoka katika ardhi kila mnyama wa msituni, na kila ndege wa angani, akamletea Adamu ili aone atawaitaje; kila kiumbe hai, jina alilokiita Adamu likawa ndilo jina lake.
Utoe pamoja nawe kila kilicho hai kilichomo pamoja nawe, chenye mwili, ndege, na mnyama, na kila kitambaacho, chenye kutambaa juu ya nchi; wajae katika nchi, wawe na uzazi, wakaongezeke katika nchi.
Huyameesha majani kwa makundi, Na maboga kwa matumizi ya mwanadamu; Ili atoe chakula katika nchi,
na kila mahali wakaapo wanadamu, wanyama wa kondeni na ndege wa angani amewatia mkononi mwako, naye amekumilikisha juu ya hao wote; wewe u kichwa kile cha dhahabu.
na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya elfu mia moja na ishirini, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tena wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?