Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.
Zaburi 5:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako, maana maadui zangu ni wengi; uiweke njia yako wazi mbele yangu. Biblia Habari Njema - BHND Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako, maana maadui zangu ni wengi; uiweke njia yako wazi mbele yangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uniongoze, ee Mwenyezi-Mungu, katika uadilifu wako, maana maadui zangu ni wengi; uiweke njia yako wazi mbele yangu. Neno: Bibilia Takatifu Niongoze katika haki yako, Ee Mwenyezi Mungu, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Niongoze katika haki yako, Ee bwana, kwa sababu ya adui zangu, nyoosha njia yako mbele yangu. BIBLIA KISWAHILI BWANA, uniongoze kwa haki yako, Kwa sababu yao wanaoniotea. Uinyoshe njia yako mbele ya uso wangu, |
Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za BWANA nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika atakufa.
Nitasujudu nikilikabili hekalu lako takatifu, Nitalishukuru jina lako, Kwa ajili ya fadhili zako na uaminifu wako, Kwa maana umeikuza ahadi yako, na jina lako juu ya vyote.
Ee BWANA, unifundishe njia yako, Na kuniongoza katika njia iliyonyoka; Kwa sababu yao wanaoniotea;
Mungu wa fadhili zangu atanitangulia, Mungu atanijalia kutazama kwa ushindi juu ya adui zangu.
Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;
Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu; Vilindi vilinizunguka; Mwani ulikizinga kichwa changu;
Kwa sababu huyo ndiye aliyenenwa na nabii Isaya, akisema, Sauti ya mtu aliaye nyikani, Itengenezeni njia ya Bwana, Yanyosheni mapito yake.
mkaifanyie miguu yenu njia za kunyoka, ili kitu kilicho kiwete kisipotoshwe, bali afadhali kiponywe.