Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
Zaburi 5:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao uovu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wenye majivuno hawastahimili mbele yako; wewe wawachukia wote watendao maovu. Biblia Habari Njema - BHND Wenye majivuno hawastahimili mbele yako; wewe wawachukia wote watendao maovu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wenye majivuno hawastahimili mbele yako; wewe wawachukia wote watendao maovu. Neno: Bibilia Takatifu Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya. Neno: Maandiko Matakatifu Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako, unawachukia wote watendao mabaya. BIBLIA KISWAHILI Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako; Unawachukia wote watendao uovu. |
Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu.
Mpumbavu husema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.
Enyi wajinga, hata lini mtapenda ujinga? Na wenye dharau kupenda dharau yao, Na wapumbavu kuchukia maarifa?
Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.
Uovu wao wote u katika Gilgali; maana huko niliwachukia; kwa sababu ya uovu wa matendo yao nitawafukuza watoke katika nyumba yangu; sitawapenda tena; wakuu wao wote ni waasi.
Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.
Wewe uliye na macho safi hata usiweze kuangalia uovu, wewe usiyeweza kutazama ukaidi, mbona unawaangalia watendao kwa hila; na kunyamaza kimya, hapo mtu mwovu ammezapo mtu aliye mwenye haki kuliko yeye;
Nami nikawakatilia mbali wachungaji watatu katika mwezi mmoja; maana nafsi yangu ilikuwa imechoka kwa ajili yao, na nafsi zao pia walinichukia.
Kisha atawaambia na wale walioko katika mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, mwende katika moto wa milele, aliowekewa tayari Ibilisi na malaika zake;