Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.
Zaburi 5:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Biblia Habari Njema - BHND Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usikilize maneno yangu, ee Mwenyezi-Mungu, usikie ninavyopiga kite. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, tegea sikio maneno yangu, uangalie kupiga kite kwangu. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu, Ukuangalie kutafakari kwangu. |
Ee BWANA, usikie haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya hila.
Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee BWANA, Mwamba wangu, na mwokozi wangu.
Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
Wewe uchungaye Israeli, usikie, Wewe umwongozaye Yusufu kama kundi; Wewe uketiye juu ya makerubi, utoe nuru.
Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, Na masikio yake husikiliza maombi yao; Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.
Basi Hana alikuwa akinena moyoni mwake; midomo yake tu ilionekana kama anena, sauti yake isisikiwe; kwa hiyo huyo Eli alimdhania kuwa amelewa.
Usimdhanie mjakazi wako kuwa ni mwanamke asiyefaa kitu; kwa kuwa katika wingi wa kuugua kwangu na kusikitika kwangu ndivyo nilivyonena hata sasa.