Zaburi 49:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitatega sikio nisikilize methali, nitafafanua kitendawili kwa muziki wa zeze. Biblia Habari Njema - BHND Nitatega sikio nisikilize methali, nitafafanua kitendawili kwa muziki wa zeze. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitatega sikio nisikilize methali, nitafafanua kitendawili kwa muziki wa zeze. Neno: Bibilia Takatifu Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: Neno: Maandiko Matakatifu Nitatega sikio langu nisikilize mithali, nitafafanua kitendawili kwa zeze: BIBLIA KISWAHILI Nitatega sikio langu nisikie mithali, Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi. |
Ndipo nikasema, Ee Bwana MUNGU, wao hunisema; Je! Mtu huyu si mtu mwenye kupiga mithali?
Na wakati wa mwisho wa ufalme wao, wakosaji watakapotimia kilele cha uovu wao, mfalme mwenye uso mkali, afahamuye mafumbo, atasimama.
Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la BWANA yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumteta mtumishi wangu, huyo Musa?
Akatunga mithali yake, akasema, Balaki amenileta kutoka Aramu, Mfalme wa Moabu kutoka milima ya mashariki, Njoo! Unilaanie Yakobo, Njoo! Unishutumie Israeli.
ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu kuumbwa kwa ulimwengu.
Basi, yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatatangazwa juu ya dari.