Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
Zaburi 49:18 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ajapojikuza katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, Biblia Habari Njema - BHND Ajapojikuza katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ajapojikuza katika maisha haya, na kusifiwa kwa sababu ya kufanikiwa, Neno: Bibilia Takatifu Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, Neno: Maandiko Matakatifu Ingawa alipokuwa akiishi alijihesabu kuwa heri, na wanadamu wanakusifu unapofanikiwa, BIBLIA KISWAHILI Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai, Na watu watakusifu ukijitendea mema, |
Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi langoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo mfalme alivyoamuru wamfanyie. Lakini Mordekai hakumwinamia, wala kumsujudia.
Maana mdhalimu hujisifia tamaa ya nafsi yake, Na mwenye choyo humkana BWANA na kumdharau.
na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake.
Naye Efraimu alisema, Kweli nimekuwa tajiri, nimejipatia mali nyingi; katika kazi zangu zote hawataona kwangu uovu wowote uliokuwa dhambi.
Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi.
ikawa asikiapo maneno ya laana hii, ajibarikie mtu huyo moyoni mwake, na kusema, Nitakuwa katika amani, nijapotembea katika upotoe wa moyo wangu kwa kuangamiza mbichi na kavu;
na hivi ndivyo mtakavyomwambia huyu aishiye salama, Amani na iwe kwako, na amani nyumbani mwako, na amani kwao wote ulio nao.