Zaburi 49:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sikieni jambo hili enyi watu wote! Tegeni sikio enyi wakazi wote wa dunia; Biblia Habari Njema - BHND Sikieni jambo hili enyi watu wote! Tegeni sikio enyi wakazi wote wa dunia; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sikieni jambo hili enyi watu wote! Tegeni sikio enyi wakazi wote wa dunia; Neno: Bibilia Takatifu Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mnaoishi dunia hii. Neno: Maandiko Matakatifu Sikieni haya, enyi mataifa yote, sikilizeni, ninyi wote mkaao dunia hii. BIBLIA KISWAHILI Sikieni haya, enyi mataifa yote; Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani. |
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
Sikieni, enyi mbingu, tega sikio, Ee nchi, kwa maana BWANA amenena; Nimewalisha watoto na kuwalea, nao wameniasi.
naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuyainua makabila ya Yakobo, na kuwarejesha watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.
ambalo Yeremia, nabii, aliwaambia watu wote wa Yuda, na wenyeji wote wa Yerusalemu, kusema,
Sikilizeni, enyi watu wa kabila zote; sikiliza, Ee dunia, na vyote vilivyomo; Bwana MUNGU na ashuhudie juu yenu, yeye Bwana kutoka hekalu lake takatifu.
Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi.
Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi katika miisho ya ulimwengu.
Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia;
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye hatapatikana na madhara ya mauti ya pili.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa, nami nitampa jiwe jeupe, na juu ya jiwe hilo limeandikwa jina jipya asilolijua mtu ila yeye anayelipokea.
Yeye aliye na sikio, na alisikie neno hili ambalo Roho anayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa kula matunda ya mti wa uzima, ulio katika bustani ya Mungu.