Ndipo Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, Watumishi wangu na waende pamoja na watumishi wako merikebuni. Lakini Yehoshafati hakukubali.
Zaburi 48:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa BWANA wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha hata milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yote tuliyosikia tumejionea wenyewe katika mji wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, naam, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha milele. Biblia Habari Njema - BHND Yote tuliyosikia tumejionea wenyewe katika mji wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, naam, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yote tuliyosikia tumejionea wenyewe katika mji wa Mwenyezi-Mungu wa majeshi, naam, katika mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha milele. Neno: Bibilia Takatifu Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele. Neno: Maandiko Matakatifu Kama tulivyokuwa tumesikia, ndivyo tulivyoona katika mji wa bwana Mwenye Nguvu Zote, katika mji wa Mungu wetu: Mungu ataufanya uwe salama milele. BIBLIA KISWAHILI Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona, Katika mji wa BWANA wa majeshi. Mji wa Mungu wetu; Mungu atauimarisha hata milele. |
Ndipo Ahazia mwana wa Ahabu akamwambia Yehoshafati, Watumishi wangu na waende pamoja na watumishi wako merikebuni. Lakini Yehoshafati hakukubali.
Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa, Huyu na huyu alizaliwa humo. Na Yeye Aliye Juu Atauimarisha.
Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo; Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.
Wavuta makasia wako walikuleta katika maji makuu; upepo wa mashariki umekuvunja moyoni mwa bahari.
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.