Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
Zaburi 48:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama upepo wa mashariki Unapovunja jahazi za Tarshishi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kama waliokumbwa na kimbunga cha mashariki ambacho huzivunjavunja meli za Tarshishi. Biblia Habari Njema - BHND kama waliokumbwa na kimbunga cha mashariki ambacho huzivunjavunja meli za Tarshishi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kama waliokumbwa na kimbunga cha mashariki ambacho huzivunjavunja meli za Tarshishi. Neno: Bibilia Takatifu Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki. Neno: Maandiko Matakatifu Uliwaangamiza kama meli za Tarshishi zilizovunjwa na upepo wa mashariki. BIBLIA KISWAHILI Kama upepo wa mashariki Unapovunja jahazi za Tarshishi. |
Kwa kuwa mfalme alikuwa na merikebu za Tarshishi baharini pamoja na merikebu za Hiramu; mara moja katika miaka mitatu huja merikebu za Tarshishi, zikileta dhahabu, na fedha, na pembe, na nyani, na tausi.
Yehoshafati akafanya merikebu za Tarshishi ziende Ofiri kuchukua dhahabu; lakini hazikuenda; kwa maana merikebu zilivunjika huko Esion-geberi.
Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Nami nitawatawanya mbele ya adui, kama kwa upepo wa mashariki; nami nitaviangalia visogo vyao, wala si nyuso zao, siku ya msiba wao.