Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?
Zaburi 48:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walikuja wote pamoja. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafalme walikusanyika, wakaenda pamoja kushambulia. Biblia Habari Njema - BHND Wafalme walikusanyika, wakaenda pamoja kushambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafalme walikusanyika, wakaenda pamoja kushambulia. Neno: Bibilia Takatifu Wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja, Neno: Maandiko Matakatifu Wakati wafalme walipounganisha nguvu, waliposonga mbele pamoja, BIBLIA KISWAHILI Maana, tazama, wafalme walikusanyika; Walikuja wote pamoja. |
Basi mfalme wa Shamu moyo wake ukamfadhaika sana kwa ajili ya jambo hili; akawaita watumishi wake, akawaambia, Je! Hamtanionesha, ni mtu yupi miongoni mwenu aliye upande wa mfalme wa Israeli?
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.
Hata ikawa katika siku za Ahazi, mwana wa Yothamu, mwana wa Uzia, mfalme wa Yuda, Resini, mfalme wa Shamu, na Peka, mwana wa Remalia, mfalme wa Israeli, wakapanda wakaenda Yerusalemu ili kupigana nao, lakini hawakuweza kuushinda.
Yule mnyama akakamatwa, na yule nabii wa uongo pamoja naye, yeye aliyezifanya hizo ishara mbele yake, ambazo kwa hizo aliwadanganya watu wale walioipokea ile chapa ya huyo mnyama, nao hao walioisujudia sanamu yake; hao wawili wakatupwa wakiwa hai katika lile ziwa la moto liwakalo kwa kiberiti;