Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Zaburi 47:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa zaburi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwimbieni Mungu sifa kwa tenzi; maana yeye ni mfalme wa ulimwengu wote. Biblia Habari Njema - BHND Mwimbieni Mungu sifa kwa tenzi; maana yeye ni mfalme wa ulimwengu wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwimbieni Mungu sifa kwa tenzi; maana yeye ni mfalme wa ulimwengu wote. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa Mungu ni mfalme wa dunia yote, mwimbieni zaburi za sifa. BIBLIA KISWAHILI Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote, Imbeni kwa zaburi. |
Maana ghadhabu zake ni za muda mfupi tu; Radhi yake ni ya milele. Kilio huweza kuwapo usiku, Lakini furaha huja asubuhi.
Naye BWANA atakuwa Mfalme wa nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.