Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Zaburi 47:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Amewatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ametuwezesha kuwashinda watu wa mataifa, ameyaweka mataifa chini ya mamlaka yetu. Biblia Habari Njema - BHND Ametuwezesha kuwashinda watu wa mataifa, ameyaweka mataifa chini ya mamlaka yetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ametuwezesha kuwashinda watu wa mataifa, ameyaweka mataifa chini ya mamlaka yetu. Neno: Bibilia Takatifu Ametiisha mataifa chini yetu, watu wengi chini ya miguu yetu. Neno: Maandiko Matakatifu Ametiisha mataifa chini yetu watu wengi chini ya miguu yetu. BIBLIA KISWAHILI Amewatiisha watu wa nchi chini yetu, Na mataifa chini ya miguu yetu. |
Neno la BWANA kwa Bwana wangu, Uketi upande wangu wa kulia, Hadi niwafanyapo adui zako Kuwa chini ya miguu yako.
Ni nani asiyekucha wewe, Ee mfalme wa mataifa? Maana hii ni sifa yako wewe; kwa kuwa miongoni mwa wenye hekima wote wa mataifa, na katika hali yao ya enzi yote pia, hapana hata mmoja kama wewe.
Naye BWANA atakuwa Mfalme wa nchi yote; siku hiyo BWANA atakuwa mmoja, na jina lake moja.
Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.
U heri, Israeli. Ni nani aliye kama wewe, taifa lililookolewa na BWANA! Ndiye ngao ya msaada wako, Na upanga wa utukufu wako; Na adui zako watajitiisha chini yako, Nawe utapakanyaga mahali pao pa juu.
atakayeubadili mwili wetu wa unyonge, upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Kisha BWANA akawapa raha pande zote, sawasawa na hayo yote aliyokuwa amewaapia baba zao; wala katika adui zao wote hakusimama hata mtu mmoja miongoni mwao mbele zao; yeye BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao.