nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;
Zaburi 47:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, anatisha. Yeye ni Mfalme mkuu wa ulimwengu wote. Biblia Habari Njema - BHND Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, anatisha. Yeye ni Mfalme mkuu wa ulimwengu wote. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu Mkuu, anatisha. Yeye ni Mfalme mkuu wa ulimwengu wote. Neno: Bibilia Takatifu Jinsi gani alivyo wa kutisha, Mwenyezi Mungu Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! Neno: Maandiko Matakatifu Jinsi gani alivyo wa kutisha, bwana Aliye Juu Sana, Mfalme mkuu juu ya dunia yote! BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa BWANA Aliye Juu, mwenye kuogofya, Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. |
nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;
Kwa mambo ya kutisha utatujibu, Katika haki, Ee Mungu wa wokovu wetu. Wewe uliye tumaini la miisho yote ya dunia, Na la bahari iliyo mbali sana,
Mungu ni mwenye kutisha Kutoka patakatifu pako. Ndiye Mungu wa Israeli; Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo. Na ahimidiwe Mungu.
Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.
Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;
Usiingiwe na hofu kwa sababu yao; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, yuko pamoja nawe, Mungu mkuu, mwenye utisho.