Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
Zaburi 45:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Anapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Pia watapelekwa kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi, anaongozwa kwa mfalme, akisindikizwa na wasichana wenzake; nao pia wanapelekwa kwa mfalme. Biblia Habari Njema - BHND Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi, anaongozwa kwa mfalme, akisindikizwa na wasichana wenzake; nao pia wanapelekwa kwa mfalme. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Akiwa amevalia vazi la rangi nyingi, anaongozwa kwa mfalme, akisindikizwa na wasichana wenzake; nao pia wanapelekwa kwa mfalme. Neno: Bibilia Takatifu Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako. Neno: Maandiko Matakatifu Anaongozwa kwa mfalme, akiwa amevalia mavazi yaliyotariziwa, mabikira wenzake wanamfuata na wanaletwa kwako. BIBLIA KISWAHILI Anapelekwa kwa mfalme Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri. Wanawali wenzake wanaomfuata, Pia watapelekwa kwako. |
Na kwa lile lango la ua patakuwa na kisitiri cha dhiraa ishirini, kitakuwa cha nguo ya rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa, kazi ya mshonaji taraza; nguzo zake zitakuwa nne, na vitako vyake vinne.
Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wenye kunakishiwa vizuri.
Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe.
Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe?
Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame. Kwani mnataka kumtazama Mshulami, Kama kutazama ngoma ya Mahanaimu?
Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami popote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu.
Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa niliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi.
Je! Hawakupata mateka na kuyagawanya, Kijakazi, vijakazi wawili, kwa kila mtu? Kwa Sisera nyara ya mavazi ya rangi mbalimbali, Nyara za mavazi ya rangi mbalimbali ya darizi; Ya rangi mbalimbali ya darizi, pande zote mbili, Juu ya shingo za hao mateka.