Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
Zaburi 45:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na watu wa Tiro wanakushawishi kwa zawadi, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Tiro watakuletea zawadi; matajiri watataka upendeleo wako. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Tiro watakuletea zawadi; matajiri watataka upendeleo wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Tiro watakuletea zawadi; matajiri watataka upendeleo wako. Neno: Bibilia Takatifu Binti Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. Neno: Maandiko Matakatifu Binti wa Tiro atakuletea zawadi, watu wenye utajiri watatafuta upendeleo wako. BIBLIA KISWAHILI Na watu wa Tiro wanakushawishi kwa zawadi, Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako. |
Wakwasi wote wa dunia watakula na kusujudu, Humwinamia wote washukao mavumbini; Naam, yeye asiyeweza kujihuisha nafsi yake,
Wafalme wa Tarshishi na visiwa na walete kodi; Wafalme wa Sheba na Seba na watoe vipawa.
Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za, magenge Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako unapendeza.
Na wafalme watakuwa baba zako walezi, na malkia zao mama zako walezi; watainama mbele yako kifudifudi, na kuramba mavumbi ya miguu yako; nawe utajua ya kuwa mimi ni BWANA, tena waningojeao hawatatahayarika.
Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu, uvumba na manemane.