Na Sedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, BWANA asema hivi, Kwa hizo utawasukuma Washami, hata waharibike.
Zaburi 44:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu; Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kwa nguvu yako twawashinda maadui zetu, kwa jina lako twawakanyaga wanaotushambulia. Biblia Habari Njema - BHND Kwa nguvu yako twawashinda maadui zetu, kwa jina lako twawakanyaga wanaotushambulia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kwa nguvu yako twawashinda maadui zetu, kwa jina lako twawakanyaga wanaotushambulia. Neno: Bibilia Takatifu Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa uwezo wako tunawasukuma nyuma watesi wetu; kwa jina lako tunawakanyaga adui zetu. BIBLIA KISWAHILI Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu; Kwa jina lako tutawakanyaga watupingao. |
Na Sedekia mwana wa Kenaana akajifanyia pembe za chuma, akasema, BWANA asema hivi, Kwa hizo utawasukuma Washami, hata waharibike.
Kwa maana BWANA ndiye mwamuzi wetu; BWANA ndiye mfanya sheria wetu; BWANA ndiye mfalme wetu; ndiye atakayetuokoa.
Nikamwona huyo kondoo dume akisukuma upande wa magharibi, na upande wa kaskazini, na upande wa kusini; wala hakuna mnyama yeyote awezaye kusimama mbele yake, wala hakuna mnyama yeyote awezaye kupokonya mkononi mwake; lakini alitenda kama alivyopenda mwenyewe, akajitukuza nafsi yake.
Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu BWANA yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa.
Naye Mungu wa amani atamponda Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.]
Mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wake mume, enzi ni yake; Na pembe zake ni pembe za nyati; Kwa hizo atayasukuma mataifa yote, hata ncha za nchi; Nao ni makumi ya maelfu ya Efraimu, Nao ni maelfu ya Manase.