Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;
Zaburi 42:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu! Biblia Habari Njema - BHND Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama paa atamanivyo maji ya kijito, ndivyo ninavyokutamani, ee Mungu wangu! Neno: Bibilia Takatifu Kama ayala anavyoonea shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu inavyokuonea shauku, Ee Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kama vile ayala aoneavyo shauku vijito vya maji, ndivyo nafsi yangu ikuoneavyo shauku, Ee Mungu. BIBLIA KISWAHILI Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu. |
Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;
Ee Mungu, tumesikia kwa masikio yetu Baba zetu wametuambia, Matendo uliyoyatenda siku zao, siku za kale.
Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Bwana ndiye aliye mkuu, Na mwenye kusifiwa sana. Katika mji wa Mungu wetu, Katika mlima wake mtakatifu.
Basi Kora, mwana wa Ishari, mwana wa Kohathi, mwana wa Lawi, akatwaa watu, pamoja na Dathani na Abiramu, wana wa Eliabu, na Oni, mwana wa Pelethi, waliokuwa wana wa Reubeni;
nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza, na watu wa nyumba zao na wote walioshikamana na Kora, na vyombo vyao vyote.