Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Zaburi 4:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza. Biblia Habari Njema - BHND Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tetemekeni kwa hofu na msitende dhambi; tafakarini vitandani mwenu na kunyamaza. Neno: Bibilia Takatifu Katika hasira yako, usitende dhambi. Tulieni kimya mkiwa vitandani mwenu, mkiichunguza mioyo yenu. Neno: Maandiko Matakatifu Katika hasira yako, usitende dhambi. Mkiwa vitandani mwenu, mtulie kimya mkiichunguza mioyo yenu. BIBLIA KISWAHILI Muwe na hofu wala msitende dhambi, Tafakarini vitandani mwenu na kutulia. |
Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake.
Je! Hamniogopi mimi? Asema BWANA; hamtatetemeka mbele za uso wangu; mimi niliyeweka mchanga kuwa mpaka wa bahari, kwa amri ya daima, isiweze kuupita? Mawimbi yake yajapoumuka-umuka, hayawezi kushinda nguvu; yajapovuma sana, hayawezi kuupita.
Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake.
Jichunguzeni wenyewe muone kama mmekuwa katika imani; jithibitisheni wenyewe. Au hamjijui wenyewe, kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Isipokuwa iwe mmekataliwa.