ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
Zaburi 39:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.” Biblia Habari Njema - BHND Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilisema: “Nitayachunga maisha yangu, nisije nikatenda dhambi kwa usemi wangu. Nitafunga mdomo wangu waovu wawapo karibu nami.” Neno: Bibilia Takatifu Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” Neno: Maandiko Matakatifu Nilisema, “Nitaziangalia njia zangu na kuuzuia ulimi wangu usije ukatenda dhambi; nitaweka lijamu kinywani mwangu wakati wote waovu wanapokuwa karibu nami.” BIBLIA KISWAHILI Nilisema, Nitazitunza njia zangu Nisije nikakosa kwa ulimi wangu; Nitajitia lijamu kinywani, Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu. |
ili BWANA afanye imara neno lake alilonena kuhusu habari yangu, akisema, Ikiwa watoto wako wataiangalia njia yao, wakienda mbele zangu kwa kweli, kwa moyo wao wote, na kwa roho yao yote, (akasema), hutakosa mtu katika kiti cha enzi cha Israeli.
Lakini Yehu hakuangalia, aende katika sheria ya BWANA, Mungu wa Israeli, kwa moyo wake wote; hakutoka katika makosa ya Yeroboamu, ambayo kwa hayo aliwakosesha Israeli.
na pamoja nao Hemani na Yeduthuni, na wale wengine waliochaguliwa, waliotajwa majina yao, ili kumshukuru BWANA, kwa kuwa fadhili zake ni za milele;
Lakini yeye akamwambia, Wewe wanena kama mmoja wa hao wanawake wapumbavu anenavyo. Je! Tupate mema mkononi mwa Mungu, nasi tusipate na mabaya? Katika mambo hayo yote Ayubu hakufanya dhambi kwa midomo yake.
Waliosema, Kwa ndimi zetu tutashinda; Midomo yetu ni yetu wenyewe, Ni nani aliye bwana juu yetu?
Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Mtu akidhani ya kuwa anayo dini, wala hauzuii ulimi wake kwa hatamu, ili hali akijidanganya moyo wake, dini yake mtu huyo haifai.