Zaburi 38:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Biblia Habari Njema - BHND Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimepindika mpaka chini na kupondeka; mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Neno: Bibilia Takatifu Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. Neno: Maandiko Matakatifu Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza. BIBLIA KISWAHILI Nimejipinda na kuinama sana, Mchana kutwa ninaenda nikiomboleza. |
Mwili wangu unavikwa mabuu na madongoa ya udongo; Ngozi yangu hufumba, kisha ikatumbuka tena.
Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.
Nilisikitika kana kwamba ni rafiki au ndugu yangu, Niliinama nikilia kama aliyefiwa na mamaye.
Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumainie Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Nitamwambia Mungu, mwamba wangu, Kwa nini umenisahau? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
Kwa kuwa Wewe ndiwe Mungu uliye nguvu zangu; kwa nini umenitupa? Kwa nini ninakwenda nikihuzunika, adui wakinionea?
Wameweka wavu ili kuninasa miguu; Nimevunjika moyo; Wamechimba shimo njiani mwangu; Lakini wao wenyewe wametumbukia humo!
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso BWANA, ninakuita kila siku; Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.
Kama mbayuwayu au korongo ndivyo nilivyolia; Niliomboleza kama hua; macho yangu yamedhoofu kwa kutazama juu; Ee BWANA, nimeonewa, na uwe mdhamini wangu.