Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.
Zaburi 38:20 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nilifuata lililo jema. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu, wananipinga kwa sababu natenda mema. Biblia Habari Njema - BHND Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu, wananipinga kwa sababu natenda mema. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao wanaonilipa maovu kwa wema wangu, wananipinga kwa sababu natenda mema. Neno: Bibilia Takatifu Wanaolipa wema wangu kwa maovu hunisingizia ninapofuata lililo jema. Neno: Maandiko Matakatifu Wanaolipa maovu kwa wema wangu hunisingizia ninapofuata lililo jema. BIBLIA KISWAHILI Naam, wakilipa mabaya kwa mema, Huwa adui zangu kwa kuwa nilifuata lililo jema. |
Uitoe nafsi yangu kifungoni. Nipate kulishukuru jina lako. Wenye haki watanizunguka, Kwa kuwa Wewe unanikirimu.
Ikiwa nimemlipa mabaya Yeye aliyekaa kwangu salama; (Hasha! Nimemponya yeye Aliyekuwa mtesi wangu bila sababu;)
Je! Mabaya yalipwe badala ya mema? Maana wameichimbia nafsi yangu shimo. Kumbuka jinsi nilivyosimama mbele zako, ili niseme mema kwa ajili yao, nikaigeuze ghadhabu yako isiwapate.
Yesu akawajibu, Kazi njema nyingi nimewaonesha, zitokazo kwa Baba; kwa ajili ya kazi ipi katika hizo mnanipiga kwa mawe?
si kama Kaini alivyokuwa wa yule mwovu, akamwua ndugu yake. Naye alimwua kwa sababu gani? Kwa sababu matendo yake yalikuwa mabaya, na ya ndugu yake yalikuwa ya haki.
Ndipo Daudi akasema, Je! Watu wa Keila watanitia mimi na watu wangu mkononi mwake Sauli? BWANA akasema, Watakutia.
Ndipo wakaenda Keila, Daudi na watu wake, wakapigana na hao Wafilisti, wakateka nyara ng'ombe zao, na kuwaua uuaji mkuu. Hivyo Daudi akawaokoa watu wa Keila.
watu hao walikuwa boma kwetu usiku na mchana, wakati wote tulipokuwa nao tukiwachunga kondoo.
Basi Daudi alikuwa amesema, Hakika ni bure nilivyokuwa nikilinda nyikani yote aliyo nayo mtu huyu, asipotewe na kitu chochote cha mali yake yote; naye amenilipa mabaya badala ya mema.