Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Zaburi 38:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mishale yako imenichoma; mkono wako umenigandamiza. Biblia Habari Njema - BHND Mishale yako imenichoma; mkono wako umenigandamiza. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mishale yako imenichoma; mkono wako umenigandamiza. Neno: Bibilia Takatifu Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenipiga. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana mishale yako imenichoma, Na mkono wako umenipata. |
Kwa kuwa mishale ya huyo Mwenyezi iko ndani yangu, Na roho yangu inainywa sumu yake; Vitisho vya Mungu vimejipanga juu yangu.
Kwa maana mchana na usiku Mkono wako ulinilemea. Jasho langu likakauka hata nikawa Kama nchi kavu wakati wa kaskazi.
Tena mkono wa BWANA ulikuwa juu yao ili kuwaangamiza, kuwatoa katika kambi hadi walipouwawa.
je! Mngesubiri hata watakapokuwa watu wazima? Mngejizuia msiwe na waume? La, sivyo, wanangu; maana ni vigumu kwangu kuliko kwenu, kwa sababu mkono wa BWANA umetoka juu yangu.
Kwa hiyo wakatuma watu waende kuwakusanya wakuu wote wa Wafilisti, wakasema, Liondoeni hilo sanduku la Mungu wa Israeli, liende tena mahali pake, ili lisituue sisi, wala watu wetu; kwa sababu kulikuwa na fadhaa kubwa sana mjini kote; mkono wa Mungu ulikuwa mzito mno huko.
Lakini mkono wa BWANA ulikuwa mzito juu ya watu wa Ashdodi, akawaangamiza, akawapiga kwa majipu, huko Ashdodi na mipakani mwake.
Kisha angalieni, likikwea kwa njia ya mpakani mwake kwenda Beth-shemeshi, basi, ndiye aliyetutenda uovu huo mkuu; la, sivyo, ndipo tutakapojua ya kwamba si mkono wake uliotupiga; ilikuwa ni bahati mbaya iliyotupata.