Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu.
Zaburi 38:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Rafiki na wenzangu wanaepa kuona mateso yangu, na jamaa zangu wanakaa mbali nami. Biblia Habari Njema - BHND Rafiki na wenzangu wanaepa kuona mateso yangu, na jamaa zangu wanakaa mbali nami. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Rafiki na wenzangu wanaepa kuona mateso yangu, na jamaa zangu wanakaa mbali nami. Neno: Bibilia Takatifu Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani wangu wanakaa mbali nami. Neno: Maandiko Matakatifu Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani zangu wanakaa mbali nami. BIBLIA KISWAHILI Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Na jamaa zangu wanasimama mbali. |
Kwa maana mbwa wamenizunguka; Kusanyiko la waovu wamenisonga; Wamenidunga mikono na miguu.
Kwa sababu ya watesi wangu nimelaumiwa, Naam, hasa kwa jirani zangu; Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu; Wanaoniona njiani wananikimbia.
Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa.
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Lakini haya yote yamekuwa, ili maandiko ya manabii yatimizwe. Ndipo wanafunzi wote wakamwacha, wakakimbia.
Wakamkamata, wakamchukua, wakaenda naye nyumbani kwa Kuhani Mkuu. Na Petro alimfuata kwa mbali.
Na wote waliojuana naye, na wale wanawake walioandamana naye toka Galilaya, wakasimama kwa mbali, wakitazama mambo hayo.
Tazama, saa inakuja, naam, imekwisha kuja, ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; lakini mimi siko peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami.