Zaburi 38:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Moyo wangu unadundadunda, Nguvu zangu zimenitoka; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia. Biblia Habari Njema - BHND Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Moyo wanidunda, nguvu zimeniishia; hata macho yangu nayo yamekwisha fifia. Neno: Bibilia Takatifu Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. Neno: Maandiko Matakatifu Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza. BIBLIA KISWAHILI Moyo wangu unadundadunda, Nguvu zangu zimenitoka; Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka. |
Maana maisha yangu yamekwisha kwa huzuni, Na miaka yangu kwa maumivu. Nguvu zangu zimeniishia kwa uovu wangu, Na mifupa yangu imepooza.
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
Nimechoka kwa kulia kwangu, Koo yangu imekauka. Macho yangu yamedhoofika Kwa kumngoja Mungu wangu.
Jicho langu limefifia kwa ajili ya mateso BWANA, ninakuita kila siku; Ninakunyoshea Wewe mikono yangu.
Moyo wangu unapigapiga, utisho umenitaabisha, gizagiza la jioni nilipendalo limegeuka likanitetemesha.
Macho yangu yamechoka kwa machozi, Mtima wangu umetaabika; Ini langu linamiminwa juu ya nchi Kwa uharibifu wa binti ya watu wangu; Kwa sababu watoto wachanga na wanyonyao, Huzimia katika mitaa ya mji.