Zaburi 38:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, usinikemee kwa hasira yako; usiniadhibu kwa ghadhabu yako. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako. BIBLIA KISWAHILI Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako, Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako. |
Umemwadhibu kwa kiasi, ulipomfukuza; ukampepeta kwa upepo mkali katika siku ya upepo wa mashariki.
Kwa ghadhabu ifurikayo nilikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema BWANA, Mkombozi wako.
Maana mimi ni pamoja nawe, asema BWANA, nikuokoe; maana nitawakomesha kabisa mataifa yote huko nilikokutawanya, bali sitakukomesha wewe kabisa; lakini nitakurudi kwa hukumu, wala sitakuacha bila adhabu.
Ee BWANA, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee BWANA, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.
Kwa kuwa niliogopa hasira na makamio aliyowakasirikia BWANA kutaka kuwaangamiza. Lakini BWANA alinisikiza wakati huo nao.