Zaburi 37:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu watendao mabaya wataangamizwa, bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi. Biblia Habari Njema - BHND Watu watendao mabaya wataangamizwa, bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu watendao mabaya wataangamizwa, bali wanaomtumaini Mwenyezi-Mungu wataimiliki nchi. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini Mwenyezi Mungu watairithi nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana waovu watakatiliwa mbali, bali wale wanaomtumaini bwana watairithi nchi. BIBLIA KISWAHILI Maana watenda mabaya watakatiliwa mbali, Bali wamngojao BWANA ndio watakaoirithi nchi. |
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Utakapolia, na wakuponye hao uliowakusanya; lakini upepo utawachukua; uvuvio tu utawachukulia mbali; lakini yeye anayenitumaini ataimiliki nchi, na kuurithi mlima wangu mtakatifu.
ndipo utakapojifurahisha katika BWANA; nami nitakupandisha mahali pa nchi palipoinuka; nitakulisha urithi wa Yakobo baba yako; kwa maana kinywa cha BWANA kimenena hayo.
Watu wako nao watakuwa wenye haki wote, Nao watairithi nchi milele; Wao ni chipukizi nililolipanda mimi mwenyewe, Kazi ya mikono yangu mwenyewe, Ili mimi nitukuzwe.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.
Lakini sasa wanaitamani nchi iliyo bora, yaani, ya mbinguni. Kwa hiyo Mungu haoni haya kuitwa Mungu wao; maana amewatengenezea mji.
Kisha Musa akaniapia siku hiyo, akasema, Hakika hiyo nchi ambayo miguu yako imekanyaga itakuwa ni urithi kwako wewe, na kwa watoto wako milele, kwa sababu wewe umemfuata BWANA, Mungu wako, kwa utimilifu.