Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Zaburi 37:25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzawa wake akiomba chakula. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula. Biblia Habari Njema - BHND Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au: watoto wake wakiombaomba chakula. Neno: Bibilia Takatifu Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. Neno: Maandiko Matakatifu Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, lakini sijaona kamwe wenye haki wameachwa au watoto wao wakiombaomba chakula. BIBLIA KISWAHILI Nilikuwa kijana na sasa ni mzee, Lakini sijamwona mwenye haki ameachwa Wala mzao wake akiomba chakula. |
Agano langu nitalifanya imara kati yangu na wewe, na uzao wako baada yako, na vizazi vyao, kuwa agano la milele, kwamba nitakuwa Mungu kwako na kwa uzao wako baada yako.
Hutangatanga ili apate chakula, akisema, Ki wapi? Ajua kwamba siku ya giza i tayari karibu naye;
Kumbuka, tafadhali, ni nani aliyeangamia akiwa hana hatia? Au ni wapi hao waelekevu walikatiliwa mbali?
Kwa kuwa BWANA hupenda haki, Wala hawaachi watauwa wake. Wao hulindwa milele, Bali mzawa wa wasio haki ataharibiwa.
Na hata nikiwa ni mzee mwenye mvi, Ee Mungu, usiniache. Hata niwaeleze watu wa kizazi hiki nguvu zako, Na kila atakayekuja uweza wako.
Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi; Na mali ya mkosaji huwa akiba kwa mwenye haki.
Na watoto wao wachanga watavunjwavunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watanajisiwa.
Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakamchukua na Mnasoni, mtu wa Kipro, mwanafunzi wa zamani ambaye ndiye tutakayekaa kwake.
Msiwe na tabia ya kupenda fedha; muwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kamwe, wala sitakuacha.
Hakuna mtu yeyote atakayeweza kusimama mbele yako siku zote za maisha yako; kama nilivyokuwa pamoja na Musa, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe; sitakupungukia wala sitakuacha.
visivyoweza kusaidia wala kuokoa, kwa kuwa havifai kitu. Maana BWANA hatawaacha watu wake kwa ajili ya jina lake kuu; kwa kuwa imempendeza BWANA kuwafanya ninyi kuwa watu wake mwenyewe.