Zaburi 37:19 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawataaibika zikifika nyakati mbaya; siku za njaa watakuwa na chakula tele. Biblia Habari Njema - BHND Hawataaibika zikifika nyakati mbaya; siku za njaa watakuwa na chakula tele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawataaibika zikifika nyakati mbaya; siku za njaa watakuwa na chakula tele. Neno: Bibilia Takatifu Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. Neno: Maandiko Matakatifu Siku za maafa hawatanyauka, siku za njaa watafurahia wingi wa vitu. BIBLIA KISWAHILI Hawataaibika wakati wa ubaya, Na siku za njaa watashiba. |
BWANA hataiacha nafsi ya mwenye haki ife na njaa; Bali tamaa ya mtu mwovu huisukumia mbali.
Maana mwanadamu naye hajui wakati wake; kama samaki wanaokamatwa katika nyavu mbaya, na mfano wa ndege wanaonaswa mtegoni, kadhalika wanadamu hunaswa katika wakati mbaya, unapowaangukia kwa ghafla.
Huyu ndiye atakayekaa juu; majabali ni ngome yake; atapewa chakula chake; maji yake hayatakoma.
Kwa ajili ya hayo mwenye busara atanyamaza kimya wakati kama huo; kwa kuwa ni wakati mbaya.
Basi BWANA asema hivi, Angalia, nakusudia jambo baya juu ya jamaa hii, ambalo hamtazitoa shingo zenu, wala hamtakwenda kwa kiburi; kwa maana ni wakati mbaya.