Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
Zaburi 36:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kumbe watendao maovu wameanguka; wameangushwa chini, hawawezi kuinuka. Biblia Habari Njema - BHND Kumbe watendao maovu wameanguka; wameangushwa chini, hawawezi kuinuka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kumbe watendao maovu wameanguka; wameangushwa chini, hawawezi kuinuka. Neno: Bibilia Takatifu Tazama jinsi watenda maovu walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka! Neno: Maandiko Matakatifu Angalia jinsi watenda mabaya walivyoanguka: wametupwa chini, hawawezi kuinuka! BIBLIA KISWAHILI Huko ndiko walikoanguka wafanyao maovu; Wameangushwa chini wasiweze kusimama. |
Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni, Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
nawe utasema, Hivyo ndivyo utakavyozama Babeli, wala hautazuka tena, kwa sababu ya mabaya yote nitakayoleta juu yake; nao watachoka. Maneno ya Yeremia yamefika hata hapa.
Ni nani asiyekucha, Ee Bwana, na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako u Mtakatifu; kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele zako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
Na waangamie vivyo hivyo adui zako wote, Ee BWANA. Bali wao wampendao na wawe kama jua hapo litokapo kwa nguvu zake. Nayo nchi ikastarehe miaka arubaini.