Zaburi 35:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Waache hao wanaofurahia maafa yangu, washindwe wote na kufedheheka. Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi, waone haya na kuaibika. Biblia Habari Njema - BHND Waache hao wanaofurahia maafa yangu, washindwe wote na kufedheheka. Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi, waone haya na kuaibika. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Waache hao wanaofurahia maafa yangu, washindwe wote na kufedheheka. Hao wote wanaojiona wema kuliko mimi, waone haya na kuaibika. Neno: Bibilia Takatifu Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau. Neno: Maandiko Matakatifu Wote wanaofurahia dhiki yangu waaibishwe na wachanganyikiwe; hao wanaojiinua dhidi yangu wavikwe aibu na dharau. BIBLIA KISWAHILI Waaibishwe, wafedheheshwe pamoja, Wanaoifurahia hali yangu mbaya. Wavikwe aibu na fedheha, Wanaojikuza juu yangu. |
Waaibike na kufedheheka, Wanaoitafuta nafsi yangu. Warudishwe nyuma, wafadhaishwe, Wanaonizulia mabaya.
Maana nilisema, Wasije wakanifurahia; Wale wanaojitukuza juu yangu Mguu wangu unapoteleza.
Kwa maana si adui aliyenitukana; Kama ndivyo, ningevumilia. Aliyejitukuza juu yangu siye anichukiaye; Kama ndivyo, ningejificha asinione.
Tazama, wote walioona hasira juu yako watatahayarika na kufadhaika; watu washindanao nawe watakuwa si kitu, na kuangamia.
Lakini BWANA yuko pamoja nami, mfano wa shujaa mwenye kutisha; kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda; watatahayarika sana. Kwa sababu hawatafaulu wataona aibu ya milele, ambayo haitasahauliwa kamwe.
na Moabu atagaagaa katika matapiko yake, naye atadhihakiwa. Kwa maana Israeli, je! Hakuwa dhihaka kwako?
Naye mfalme atafanya kama apendavyo; naye atajitukuza na kujiadhimisha juu ya kila mungu, naye atanena maneno ya ajabu juu ya Mungu wa miungu, naye atafanikiwa mpaka ghadhabu itakapotimia; maana yaliyokusudiwa yatafanyika.
Ndipo adui yangu ataliona jambo hilo, na aibu itamfunika, yeye aliyeniambia, Yuko wapi BWANA, Mungu wako? Macho yangu yatamtazama; sasa atakanyagwa kama matope ya njia kuu.
Vivyo hivyo ninyi vijana, watiini wazee. Naam, ninyi nyote jifungeni unyenyekevu, mpate kuhudumiana; kwa sababu Mungu huwapinga wenye kiburi, lakini huwapa wanyenyekevu neema.